WAJUMBE wa bodi ya Mfuko wa Rais wa kujitegemea uwezeshaji kiuchumi wakiongozwa na Mwenyekiti wa bodi NATU MSUYA wakitembelea vikundi vya wajasiriamali wilaya Lindi
WAJUMBE wa bodi ya Mfuko wa Rais wa kujitegemea uwezeshaji kiuchumi wakitembelea vikundi vya wajasiriamali TOP FIVE Mkwaya wilaya Lindi
WAJUMBE wa bodi ya Mfuko wa Rais wa kujitegemea uwezeshaji kiuchumi wakitembelea vikundi vya wajasiriamali HIJI wilaya Lindi
WAJUMBE wa bodi ya Mfuko wa Rais wa kujitegemea uwezeshaji kiuchumi wakionozwa na mwenyekiti NATU MSUYA wakitembelea vikundi vya wajasiriamali wilaya Lindi
WAJUMBE wa bodi ya Mfuko wa Rais wa kujitegemea uwezeshaji kiuchumi wakiongozwa na mwenyekiti NATU MSUYA wakitembelea vikundi vya wajasiriamali wilaya Lindi
kukosekana kwa umeme wa uhakika mkoani Lindi kumeelezwa kuwa kunachangia Wajasiriamali kushindwa kufikia malengo yao ya uzalishaji
Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya wafanyabiashara wakati walipokuwa wanatoa taarifa za za vikundi kwa bodi ya mfuko wa Rais wa kujitegemea walipokuwa kwenye ziara ya kutembelea vikundi vilivyokopeshwa mikopo kupitia mfuko huo
Akisoma taarifa hiyo mwenyekiti wa kikundi cha HIJI WORK SHOP, Hiji Twalibu timu ya alisema tatizo la kukosekana kwa huduma ya wa uhakika unachangia kiwanda kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji na kusabisha mapato kuwa madogo
Twalibu alisema kuwa imekuwa utamaduni wa kawaida kuona umeme haupatika siku mzima baadhi ya maeneo yakipata huduma hiyo kwa mashaka na kiasi kidogo ikiambatana na mgawo na kukatika katika kusiko weza kuelezwa.
Alisema umekuwa tatizo sababu baadhi wamekuwa wakipata huduma hiyo usiku wa manane na alfajiri umeme unakatwa jambo ambalo limesababisha malalamiko mengi ya wateja .
Zakia Litonji alisema shirika la umeme mkoani humu limeshindwa kutoa huduma kwa wakati na kusababisha usumbufu kwao na wakosesha mapato ambayo wanayatumia kulipa kodi kwenye mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)
Kwa upande Afisa Habari wa Tenesco mkoa wa Lindi Francis Mbelwa alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na alisema hivi sasa huduma hiyo ya umeme inatolewa kwa mgawo kwa sababu uwezo wa ufuaji wa umeme umepungua kutokana na kuharibika kwa Generata moja iliyoko mkoa Mtwara kwenye kituo cha kufulia umeme.
Mbelwa alisema tatizo litaondoka baada ya kuletwa genarate mpya mbili zilizoombwa ili kuongea nguvu ya uzalishaji uvuaji umeme kwenye kituo cha kugawa umeme mikoa ya Lindi na Mtwara
Awali Afisa Mikopo tawi la Lindi Zeitun Halfan alitoa taarifa kwa bodi hiyo kuwa mfuko tawi la Lindi umefanikiwa kutoa mikopo 144 yenye thamani ya shs milioni 73 kati hiyo mikopo 30 yenye thamani ya shs milioni 13,100,000 imetolewa kwa vijana , na mikopo 114 yenye thamani ya shs milioni 69 900,000 zimetolewa kwa wanawake na mikopo 29 yenye thamani ya shs milioni 10,800,000 kwa vikundi nne vya wajasilimali wanawake wilaya Ruangwa.
Zeitun alisema vikundi 87 vyenye wajasilimari 165, vijana 35 na wanawake 130 zilivyoko wilaya Lindi na Ruangwa vinajishughulisha katika shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji,utengenezaji wa sabuni na vikapu,na wilaya Lindi, vinajihusisha, kilimo, bustani,ufugaji wa kuku, mashamba ya chumvi, ushonaji, na uselemara.

Post a Comment