Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Dar es Salaam Young Africans leo Jumapili ya August 27 2017 imeingia uwanjani kucheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 dhidi ya Lipuli FC ya
Iringa.
Yanga ambao ndio Mabingwa watetezi wa tajili la VPL baada ya kuchukua kwa mara ya tatu mfululizo, wamekutana na upinzania usio wa kawaida na kulazimishwa sare ya kufunga goli 1-1, Lipuli FC ikiwa ndio imepanda daraja msimu huu.
Licha ya kuwa Lipuli FC imepanda daraja na kufanya usajili wa gharama nafuu tofauti na baadhi ya vilabu vya Ligi Kuu wamefanikiwa kuidhibiti
Yanga isiguse nyavu zao na hatimae wakaishia goli lao moja la kusawazisha lililofungwa na Donald Ngoma dakika ya 45+2 baada ya Seif Karihe kufunga goli la uongozi kwa
Lipuli FC dakika ya 45.
Post a Comment