Gwaride
la ukakamavu la wanafunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari ya
Jitegemee JKT Mgulani likipita mbele ya mgeni rasmi katika hafla
iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.
Gwaride lilipita jukwaa kuu.
Meza kuu ikitoa Saluti wakati gwaride likipita mbele yao.
Maofisa wa Jeshi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mmoja
wa makamanda wa gwaride hilo, Ibrahim Mrisho akipongezwa na mgeni rasmi
baada ya kupokea zawadi yake. Ibrahim alikuwa miongoni mwa makanda sita
waliozawadiwa kwa kufanya vyema kwenye gwaride hilo, wengine ni Moses
Peter, Azan Mohamed, Kidali Saidi na Clementina Joseph.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegeme, Robert Kessy akizungumza
Kanali
Emanuel Mwaigobeko ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Makongo
inayomilikiwa na jeshi akimpongeza mgeni rasmi Mgombolwa kwa hotuba
nzuri aliyoitoa kwa wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ukakamavu.
Gadi ya wasichana ikiwa imetulia wakari wa hafla hiyo.
Mgeni rasmi akipiga saluti wakati akipokea heshima wakati gwaride hilo lililopita mbele yake.
Brass Bendi ya JKT iliwajibika ipasavyo wakati wa kufungwa kwa mafunzo hayo ya ukakamavu.
Na Dotto Mwaibale
KANALI
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Anchila Kagombola ambaye ni
Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Kujenga Taifa Makao Makuu
jijini Dar es Salaam, amewaasa wanafunzi kutumia mitandao ya kijamii kwa
ajili ya kujifunza na siyo kutumiana jumbe zisizofaa zinazoweza
kuhatarisha maisha yao.
Kagombola
aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya kufunga mafunzo ya ukakamavu ya
Kidato cha Tano kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee JKT High
School 2017, alitoa rai hiyo jana.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Kagombola aliwapongeza wanafunzi wa Jitegemee kwa
kujiunga na shule hiyo inayotoa elimu bora na kusisitiza ukakamavu,
maadili, uzalendo,umoja na nidhamu kwa jumla.
Kanali
Kagombola, amewaasa wanafunzi hao watumie mitandao ya kijamii kwa
kujifunza na siyo kutumiana jumbe hatarishi kwa ajili ya usalama wao na
usalama wa taifa.
“Aidha,
niwahusie wanafunzi wote wa shule hii kuwa mkwepe vishawishi vyote vya
ujana, msome kwa bidii, muache kutazama nafsi zenu hasa watoto wangu wa
kike na kupata faraja, kwani zaweza kukatisha ndoto zenu, hivyo
muwakatae wote wanaowashawishi kuingia kwenye mienendo hatarishi, mfano
kufanya ngono, utumiaji wa madawa na vitendo vya uhalifu.
Aidha,
mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Youtube na mingine itumike
kwa ajili ya kujifunza, siyo kutumiana jumbe hatarishi kwenu na kwa
usalama wa nchi. Tafadhali sana, mmenisikia?”
Kagombola
ametoa pongezi kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee, Luteni
Kanali Robert Kessy kwa kuendesha mafunzo hayo ya ukakamavu kwa
wanafunzi wa kidato cha kwanza, kidato cha tano na kwa wahamiaji.
Alibainisha
kuwa katika mtazamo wa nje mafunzo ya ukakamavu huonekana hayana
umuhimu kwa walengwa, lakini yanasaidia vijana kuishi kwa nidhamu wawapo
shuleni na uraiani na bila tabu yoyote.
“Faida
za mafunzo haya ya ukakamavu ni pamoja kudumisha nidhamu, utimamu wa
mwili, uwezo wa kufikiri haraka, uvumilivu, uadilifu, kujiamini na suala
zima la kutenda na kuamua kwa wakati ili kupata matokeo mazuri katika
masomo,” alisema Kagombola.
Hata
hivyo, ameomba mpango wa kutoa mafunzo ya ukakamavu mashuleni
uliokuwepo miaka ya nyuma urejeshwe ili kujenga ukakamavu , uzalendo na
wanafunzi kuwa na maadili.
Pia aliwasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha mtoto wa kike anapatiwa elimu bora kwa kuwa ndio walezi wa jamii.
Akizungumzia
mafunzo hayo,Luteni Kanali Kessy alisema yalianza 1985 na kwamba wakati
huo yalikuwa yakichukua wiki mbili sasa wiki tatu na yanafanyika baada
ya muda wa masomo.
‘Mafunzo haya ya ukakamavu yalianzishwa ili kuwafanya wanafunzi wawe wazalendo, wakakamavu, wenye maadili na nidhamu.
Gwaride
hilo la wanafunzi wa kidato cha tano liliongozwa na Gwaride Kamanda,
ambaye ni mwanafunzi aitwaye Zulfa Ally likihusisha wanafunzi 256 na
gadi nane.
Post a Comment