Mchezaji wa timu ya Mbaya fc akimiliki mpira kwenye mchezo dhidi ya timu ya Sido fc mchezo uliochezwa augosti 10 katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Ni moja ya vibweka vya uwanjani katika mchezo huu
Ligi ya Kazumari cup
Matokeo ya mchezo wa leo augost 10 kati ya Mbaya fc dhidi ya Sido fc umemalizika kwa timu ya Sido fc kuibuka na ushindi wa magoli 5-1 mchezo uliochezwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Katika kipindi cha kwanza timu Sido fc iliongoza magoli 2-1 na kipindi cha pili iliongeza magoli 3 katika kipindi chote cha dakika 45 za kipindi cha kwanza timu ya Mbaya fc iliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Sido fc lakini kipindi cha pili kikosi hicho kilishindwa kujipanga na nafasi hiyo Sido fc ilitumia vema kuongeza magoli 3.
Magoli ya Sido fc yalifungwa mapema namo dakika ya 3 kupitia kwa mchezaji wao Abuu Kazumari,Miraji Kikoweka dakika ya 11,Ediga Bilali dakika ya 65,Salumini Mmuka dakika ya 87 na Ramadhani Namaji aliweza kupachika goli dakika ya 89 huku goli la Mbaya fc likifungwa na Benardi Mukoleko katika dakika ya 30.
Ni moja ya vibweka vya uwanjani katika mchezo huu
Post a Comment