0
Caster SemenyaHaki miliki ya pichaPA
Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya alishinda dhahabu katika mbio za 800m upande wa wanawake siku ya mwisho ya mashindano ya ubingwa wa riadha duniani jijini London.
Bingwa huyo wa Olimpiki aliandikisha muda wa dakika moja na sekunde 55.16, muda wake bora zaidi na muda bora zaidi duniani mwaka huu.
Francine Niyonsaba wa Burundi alishinda fedha naye Ajee Wilson wa Marekani akachukua nishani ya shaba, wote wawili wakizidiwa na kasi ya kushangaza ya Semenya mita 50 za mwisho katika mbio hizo.
Mkenya Margaret Nyairera Wambui alimaliza wa nne.
Semenya, 26, amesema sasa anapanga kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 800 ambayo ni dakika moja na 53.28.
Rekodi hiyo iliwekwa na Jarmila Kratochvilova wa iliyokuwa Czechoslovakia mwaka 1983.
"Tunahitaji kuondoka kwa 1:55 kwanza na itahitaji mazoezi makali sana," amesema.
"Nina mataji ya Olimpiki, dunia na Jumuiya ya Madola kwa hivyo sasa pengine ni wakati wa kuangazia rekodi ya dunia. Ndicho kitu kinachofuata sasa kwenye orodha. Ninajua kwamba itakuwa vigumu lakini nitajaribu hivi karibuni, pengine."

Post a Comment

 
Top