Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfray Zambi amewaomba Radhi wakulima wa korosho mkoani Lindi kwa kitendo cha kukosa pembejeo ya Kilimo Sulphur kwa wakati baada ya serikali kuahidi kutoa pembejeo hizo bure
Zambi alichukua hatua hiyo baada ya Meneja wa Ubanguaji korosho kutoka bodi ya Korosho (CBT) Eng Shabani Yahaya kueleza kuwa wakulima wa korosho mkoani Lindi wasitegemee dawa zinazotolewa na bodi ya koshoro kwani hazitaweza kutosheleza , hivyo kuwataka wakulima ho kununua pembejeo hizo Madukani.
Zambi alisema kitendo cha bodi ya korosho kutangaza kusambaza dawa bure kimewafanya wakulima kuacha kununua pembejeo hizo, hali ambayo imesababisha mikorosho mingi kutopuliziwa hadi sasa.
Alisema serikali imekuwa ikitukanwa na wakulima Kila kona kutokana na utendaji mbovu wa usambaza pembejeo kwa wakulima.
wadau wa kilimo , Ufuta, Korosho , na Mihogo mkoani Lindi walikuwa kwenye kikao na Bank ya wakulima TADB wakitoa Fursa zinazotolewa na bank hiyo. Chanzo:Sauti ya kusini blog
Post a Comment