Mchezaji wa timu ya Mifugo fc akiwa anamiliki mpira kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya timu ya Wachukuzi fc mchezo uliopigwa uwanya wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
MCHEZO wa nusu fainali kati ya Mifugo fc dhidi ya Wachukuzi fc umemalizika baada ya timu ya Mifugo fc kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 na imepata tiketi ya kucheza fainali.
Katika kipindi cha kwanza timu ya Wachukuzi fc iliweza kuongoza magoli 2-1 lakini walishindwa kulinda lango lao na kurusu timu ya Mifugo fc kusawazisha goli na kuongeza goli la ziada hivyo mpaka dakika 90 za mchezo matokeo kuibuka na ushindi wa goli 3-2.
Mchezo wa kupata mshindi wa tatu utapigwa agosti 24 kati ya Vijuso Vs Wachukuzi fc na fainali kupambana agosti 25 kati ya Mitumba fc Vs Mifugo fc
ANGALIA VIDEO YA MCHEZO KATI YA MIFUGO FC Vs WACHUKUZI FC
Post a Comment