0


 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
PICHA 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
PICHA 3
Mmoja wa Wadadisi Maro D. Maro akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
PICHA 4
Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
PICHA 5
Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
……………………………………………………………………………………..
Na: Veronica Kazimoto-Dodoma

 WITO umetolewa kwa viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi watakaopita maeneo mbalimbali nchini kukusanya taarifa kwa ajili ya Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo iliyofanyika leo mkoani Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga amesema utafiti huo ni muhimu katika kunusuru kaya maskini nchini hivyo haina budi viongozi na wananchi kutoa ushirikiano kwa Wadadisi wa utafiti husika.
 
“Kwa namna ya pekee nawaomba Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri, viongozi wa kata na vijiji na wananchi wote kwa pamoja mtoe ushirikiano wa hali ya juu kwa Wadadisi watakapokuwa katika maeneo yenu wakikusanya taarifa za utafiti huu”, amesema Mwamanga.
 
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema lengo la kufanya mafunzo hayo ilikuwa ni kuwawezesha Wadadisi kufahamu taratibu zote zinazohusu kazi ya ukusanyaji taarifa na mbinu zinazotakiwa ili kupata taarifa sahihi kutoka kwenye kaya mbalimbali nchini.
 
Jumla ya Wadadisi 85 wamemaliza mafunzo ya siku 20 ya Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na TASAF.

Post a Comment

 
Top