0

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewasimamisha kazi watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, na kumuagiza katibu tawala wa mkoa huu, Ramadhan Kaswa aunde kamati ya uchunguzi.

Zambi amechukua hatua hiyo kwenye kikao maalum cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo ambacho kilipokea na kujadili ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) ya mwaka wa fedha wa 2015 /2016, kilichofanyika leo katika manispaa ya Lindi.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa watumishi ambao umechangia halmashauri hiyo kutakiwa kujibu hoja nyingi za ukaguzi kwa mujibu wa ripoti hiyo.
RC Zambi amesikitishwa na sikitishwa na kitendo cha Halmshauri hiyo kupata hati ya ukaguzi isiyo ridhisha.
Ikitakiwa kujibu hoja 36 za ukaguzi. Miongoni mwa kasoro zilizosababisha achukue hatua hiyo kwa watumishi hao ambao ni ofisa wa idara ya ushirika, ofisa ugavi na manunuzi, mhandisi wa ujenzi, mwanasheria na mhazini ni kutotolewa sababu za msingi za kushindwa kujibu hoja za ukaguzi za kila mwaka. Badala yake zimekuwa zikiongezeka.
Alisema kumekuwa na uzembe mkubwa unaosababisha hoja za ukaguzi kuendelea kuwepo kila mwaka. Huku akibainisha wazi kuwa haoni sababu ya mwanasheria wa Halmashauri hiyo kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria wa wadaiwa sugu wanaodaiwa na halmashauri hiyo.
“Lakini nashindwa kuelewa nikwanini mkaguzi wa ndani alishindwa kubainisha na kuziona kasoro hizi nakutoa ushauri hadi zimegunduliwa na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali. Miradi mingi ya ujenzi, hasa majengo yamejengwa chini ya kiwango na mhandisi yupo, matumizi ya ovyo kwasababu hayana uthibitisho fedha za kodi ya ardhi hazipelekwi benki, mabati 3000 yaliyonunuliwa hayapo stoo na mgawanyo wake hauonekani, “ amesema Zambi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi akiendelea kufafanua na kueleza sababu za kuchua  uamuzi huo aliongeza kusema mtunza hazina wa Halmashauri hiyo ameonesha udhaifu mkubwa usio vumilika. Ikiwamo kutoonekana stakabadhi za baadhi ya malipo yaliyofanyika .
“Wakionekana hawana makosa watarejea kazini, lakini sipo tayari kuvumilia na kuona uzembe kwenye halmashauri ukiendelea kufanyika, ” amesisitiza Zambi.
Baadhi ya kasoro zilizopo na zilizooneshwa  kwenye taarifa hiyo ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali ni pamoja na madai ya muda mrefu yanayofikia shilingi 669.677 milioni,madeni yanayofikia shilingi 213.484 milioni, upimaji ardhi katika eneo la Mchinga bila mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo bila kujua na uwekezaji uliochukua muda mrefu bila kutekelezwa.
Kasoro nyingine ni ununuzi wa dawa yenye thamani ya shilingi 15.38 bila fomu za maombi ya maombi ya manunuzi hayo. malipo yaliyofanywa kwa mzabuni bila kukatwa kodi ya zuio yenye jumla ya shilingi 809.31 milioni, mikaba ya miradi ya maendeleo kutopelekwa kwa mkaguzi, kamati ya ukaguzi kutokutana na mkaguzi na wajumbe wa nje wa Halmashauri ili kutatua na kuyapatia ufumbuzi mambo yaliyokosa utatuzi, kutowasilishwa na wakala jumla ya shilingi 18. 00 milioni, matumizi ya mafuta ambayo hayana udhibitisho na fedha za kodi ya ardhi shilingi 9.46 milioni.
Mengine ni malipo ya madeni ya nyuma ambayo hayaonekani kwenye orodha ya madeni yenye jumla ya shilingi 53.87.

Post a Comment

 
Top