0
Wizara ya Fedha na Mkandarasi wametiliana saini mkataba wenye thamani ya Tsh Bilioni 101 kuboresha Barabara ya Mikumi-Ifakara kwa msaada wa Umoja wa Ulaya, Marekani ‘USAID’ na Uingereza ‘UKAid’.
Katika utiaji saini wa mkataba huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaaban amesema mradi huo ni muhimu kwa sababu utaweza kuongeza uzalishaji katika kilimo na kurahisisha usafishaji wa mazao.
>>>”…katika kusaini mkataba wa ujenzi wa  barabara ya Mikumi-Ifakara ambayo ina urefu wa kilomita 67. Katika kutekeleza program yetu ya SAGCOT yaani Southern Agriculture Growth Corridor ya Tanzania.
“Mradi huu ni muhimu katika utekelezaji wa program ya SAGCOT kwa sababu utaweza kuongeza uzalishaji wa kilimo, kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka shambani hadi sokoni.” – Amina Shaaban.

Post a Comment

 
Top