0
Kikosi cha timu ya sekondari ya Liwale day kimekubali kichapo cha goli 4-2 dhidi ya wauza nguo timu ya Mitumba fc.


Mchezo wa kirafiki kati ya timu ya shule ya sekondari ya Liwale day dhidi ya Mitumba fc leo julai 14 zilipimana nguvu kimchezo wa mpira ulipigwa uwanja wa shule ya sekondari Liwale day katika mchezo huo timu ya Liwale day iliweza kupokea kichapo cha goli 4-2.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Mitumba fc ilikuwa ya kwanza kufumania lango la timu ya Liwale day kwa kuongoza magoli 3 huku timu ya Liwale day ikipumzika ikiwa haijapata hata goli.

Kindi cha pili timu ya Liwale day ilibadili mchezo na kuweza kufumania nyavu mara mbili haraka haraka magoli yaliofungwa na Hawazi Pazi huku goli la pili kifungwa na Mathias Frank lakini mabeki wa Liwale day walishindwa kulinda vema ukuta wao na kupelekea kuirusu timu ya Mitumba fc kuongeza goli la nne na matokeo kusomeka Mitumba fc 4-2.


Kwa mujibu wa kocha wa timu ya Liwale day amesema kuwa japo timu yake imefungwa lakini anauhakika mchezo ujao ataweza kulipiza kisasi hicho cha goli 4 huku akidai kikosa chake ni kipya ndio kwanza anaanza kukisuka vizuri na anamatumaini atarejesha heshima ya timu ya Liwale day kama zamani.

Post a Comment

 
Top