0
raisHaki miliki ya pichaIKULU
Image captionRais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini alipofanya ziara ya kushtukiza mwezi Machi
Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imekubali kuilipa serikali ya Tanzania nyongeza ya mrabaa wa kati ya asilimia 4 mpaka 6 kama ilivyoainishwa kwenye muswada wa sheria mpya ya madini nchini humo.
Serikali ya Tanzania na kampuni ya Acacia ziliingia katika mgogoro mapema mwezi tatu mwaka huu kutokana na kuzuiliwa kwa makontena 256 ya Mchanga wa dhahabu (makinikia) kwenye bandari ya dar es salaam baada ya kubainika kuwa Acacia haitoi taarifa sahihi ya kiwango cha madini kilichopo katika mchanga huo hivyo kulipa tozo zisizo sahihi kwa karibu miongo miwili jambo ambalo linapingwa vikali na kampuni hiyo.
Licha ya kukubali kulipa ongezeko hilo Acacia imesema bado inaendelea kutathimini athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na kuundwa kwa sheria hiyo mpya.

Post a Comment

 
Top