0
Uwanja wa mpira uliotokea maafaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUwanja wa mpira uliotokea maafa
Senegal imesimamisha shughuli zote za michezo na utamaduni kwa muda wa mwezi mmoja, siku moja tu baada ya ukuta kuanguka kwenye uwanja wa Mpira wa Miguu wa Demba Diop mjini Dakar na kusababisha vifo vya watu wanane.
Tukio hilo limetokea baada ya kutokea mapigano kati ya washabiki wa timu pinzania katika fainali za ligi nchini humo.
Kufuatia tukio hilo pia matamasha ya muziki na mashindano ya mechi mbalimbali za soka zimeahirishwa ikiwa ni sehemu ya kutambua janga hilo lililotokea.
Serikali nchini humo imepiga marufuku matukio ya aina yote ya michezo mpaka kutakapomalizika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi.
Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kile kilichoelezwa kwamba hakuna polisi wa kutosha kuweza kutoa ulinzi katika matamasha na mechi kubwa za mpira wakati huohuo wakihitajika kwenye mikutano ya kampeni za siasa.
Hata hivyo baadhi ya watu walilalamika kutokuwepo kwa polisi wa kutosha wakati vurugu hizo zilipotokea uwanjani hapo na kwamba waliokuwepo hawakuchukua uamuzi wa haraka kuzizuia.

Post a Comment

 
Top