0
Wavenezuela katika foleni ya kupiga kura ya maoni isiyo rasmiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWavenezuela katika foleni ya kupiga kura ya maoni isiyo rasmi
Mtu mmoja ameuawa nchini Venezuela wakati akisubiri kupiga kura ya maoni, katika zoezi hilo lisilo rasmi, liliyoandaliwa na upinzani dhidi ya mipango ya serikali kuandika upya katiba ya nchi hiyo.
Watu wenye silaha waliokuwa wamepanda pikipiki waliwashambulia wapiga kura nje ya kituo cha kupigia kura nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Caracas. Huku wengine watatu wakijeruhiwa.
Awali idadi kubwa ya Wavenezuela katika zaidi ya nchi mia moja walipiga kura hiyo ya maoni, ambayo Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro akiielezea kuwa isiyo na maana.
Mpaka sasa idadi kubwa ya watu wamefariki dunia katika ghasia ambazo zimeelezwa kuwa ni mbaya zaidi kuathiri uchumi wa nchi hiyo na jitihada za Rais huyo kung'ang'ania madarakani.
Tangu kuanza kwa ghasia hizo mwezi April zaidi ya watu 100 wameuawa kutokana na vurugu hizi za kisiasa.
Mwezi May mwaka huu, Rais Maduro alitoa agizo la kufanywa kwa marekebisho ya katiba, uamuzi ambao umegomewa na wapinzani kwa madai kuwa ni kinyume na demokrasia.

Post a Comment

 
Top