0
US President Donald Trump and Russian President Vladimir Putin shake hands during a meeting on the sidelines of the G20 Summit in Hamburg, Germany. July 7, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionDonald Trump na Vladimir walifanya mazungumzo katika mkutano wa G20
Viongozi kutoka vyama vyote katika bunge la Marekani wamekubaliana kuhusu sheria ambayo inaruhusu vikwazo vipya kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Sheria hiyo pia itapunguza uwezo wa Rais Donald Trump wa kuiondolea Urusi vikwazo.
Kipindi cha bwana Trump ofisini kimekumbwa na madai kuwa Urusi ilisaidia kushawishi uchaguzi wa mwaka uliopita.
Urusi inakana kutenda lolote baya la uchunguzi kadha ambao umefanywa na Marekania unatathmini ikiwa yeyote katika kampeni ya Trump alishirikiana na maafisa wa Urusi.
Waandishi wa habari wanasema kuwa makubaliano hayo ya Congress, yanaonyesha msimamo uliopo dhidi ya Urusi bila kujali maoni ya Trump.
Rais anaweza kuukataa mswada huo, lakini kwa kufanya hivyo inaweza kushukiwa kuwa anaiunga mkono Urusi.
Kwa upande mwingine ikiwa atautia sahihi itakuwa ni kuidhinisha sheria ambayo utawala wake unaipinga.
Mswada huo poia unaruhusu vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini na Iran.
Sheria hiyo itaruhusu vikwazo vipya dhidi ya Urusi kwa kulimega eneo la Crimea mwaka 2014 na madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.
A 45-acre Russian diplomatic compound, seized by the US in December 2016 in connection with suspected Russian hacking activities sits abandoned on the banks of the Corsica River near Centreville, Maryland, 10 July 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMarekani ilitwaa makao ya kidiplomasia ya Urusi kwa kuingilia uchaguzi wake


Post a Comment

 
Top