Wanafunzi wa shule ya msingi Liwale mkoani Lindi walioudhulia siku ya mtoto Afrika jana juni 16 maazimisho yalifanyika shule hapo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale,Justin MonkoAfisa maendeleo wa wilaya ya Liwale,mama Mary Ding'ohi
Wanafunzi wa shule ya msingi Liwale wakikabizi risara kwa mgeni rasmi mhe. Joseph Joseph Mkilikiti
Mgeni rasmi
mkuu wa wilayani ya Ruangwa mhe. Joseph Joseph Mkilikiti
Wazazi pamoja na jamii wilayani Liwale mkoani Lindi
wametakiwa kuwatunza watoto wao kwa kufuata maadili mema na kuwapatia
huduma zote za kimsingi ili kuweza kuwaandaa watoto hao kuwa raia wema.
Wito huo umetolewa jana juni 16 kwenye maazimisho ya
siku ya mtoto Afrika yaliyofanyika katika shule ya msingi Liwale na mgeni rasmi
mkuu wa wilayani ya Ruangwa mhe. Joseph Joseph Mkilikiti kwa niaba ya
mkuu wa wilaya wa Liwale,mhe. Sarah Chiwamba.
Jamii ina wajibu wa kushirikiana na wazazi katika
kuwalea watoto na kuondokana na zana ya mtoto ni baba na mama hivyo kila mzazi
anawajibu wa kuwalea watoto katika muongozo na kuhakikisha wazazi kuwapeleka
watoto kupata elimu.
Mkilikiti amesema viongozi wanatakiwa kuhakikisha
watoto wanaenda shule na amemwagiza kamanda wa polisi wilayani hapa kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote wasiowapeleka watoto wao
shule kupata elimu kwani wazazi wasiopenda kuwapeleka watoto wao shule wanawanyima
haki zao za kimsingi.
Maazimisho ya Mtoto Afrika mwaka 2017 likiwa limebeba kauli mbiu isemayo "Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu ya watoto katika Afrika: Kuongeza
kasi ya ulinzi, uwezeshaji na fursa sawa kwa watoto Afrika".
Post a Comment