0

Mtanzania Omega Mwaikambo ambaye anaishi Uingereza amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kupost kwenye Facebook mabaki ya mtu aliyeungua moto kwenye ajali ya moto ulioteketeza ghorofa la Grenfell Tower.

Picha hiyo iliyoamsha hisia za watu wengi ilipelekea Polisi kumkamata na kumfikisha Mahakamani kwa kosa la kuvunja faragha ya mtu aliyekufa na kupost kwenye hadhara ambapo ni kosa kisheria kufanya hivyo bila ruhusa kwa ndugu wa marehemu.

Kwa mujibu wa Polisi Mwaikambo amekiri kutenda kosa hilo lakini alijitetea kuwa alifanya hivyo kwa lengo la kuisaidia familia ya marehemu kutambua mwili wa ndugu yao ambao ulikuwa umefunikwa kwenye mfuko maalum unaotumika kuhifadhia maiti.

Mwaikambo ambaye anaishi Testerton Walk, Kusini mwa London, yadi chache kutoka kwenye jengo hilo, alikamatwa muda mfupi baada ya picha kuonekana online na kuhukumiwa miezi mitatu jela.



Post a Comment

 
Top