Wanajeshi saba wanamaji wa Marekani
hawajulikani waliko baada ya meli yao USS Fitzgerald, kugongana na meli
ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Ufilipino, katika pwani ya mashariki
mwa Japan.
Walinzi wa pwani ya Japan wametuma maboti tano na ndege mbili katika eneo hilo kusaidia katika shughuli za uokozi.
Msemaji
wa jeshi la maji la Marekani, amesema huenda maafisa hao wako sehemu za
ndani za zilizofungwa ili kuzuia maji zaidi kuingia ndani ya manuari
hiyo.
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya meli ya pili iliyokuwa na bendera ya Ufilipino ACX Crystal.
Kati ya waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa njia ya helikopta
Meli hiyo ya kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa Yokosuka.
Picha zilionyesha uharibifu mkubwa kwenye meli ya kijeshi baada ya ajali hiyo.
Haijulikani ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa ikielekea wakati huo.
Meli
ya mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa
ikipeperusha bendera ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan
ya Nagoya na Tokyo.
Post a Comment