Polisi mmoja
mwanamke amepigwa risasi kichwani wakati mwamamume mmoja alipampokonya
bunduki yake katika kituo kimoja cha treni mjini Munich.
Mwanamke
huyo alijeruhiwa vibaya pamoja na watu wawili waliokuwa kando ambao
walijeruhiwa awakti wa ufayatuaji huo wa risasi, kwa mujibu wa polisi.
Polisi walimpiga risasi na kumjeruhi mshambuliaji ambaye sasa yuko kizuizini. Polisi wanasema kuwa hakikuwa kisa cha ugaidi.
Oparesheni kubwa ya polisi inaendelea na huduma za usafiri wa reli zimesitishwa
Watu waliokuwa kando pamoja na mshukuwa hakujeruhiwa vibaya
Polisi wanasema kuwa hakuna hatari yoyote kwa umma
Post a Comment