Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani
wanaotaka marais wastaafu washitakiwe kuhusu sakata la mchanga wa
madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika
pia.
Ndugai
amesema hayo leo (June 13, 2017) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa
Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji
wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa
ya Rais.
“Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir)
Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga
ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe,” amesema Lijualikali.
Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu
walionao kwenye chama chao.
“Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena,” amesemaNdugai.
Post a Comment