Klabu
ya soka ya Chelsea imelipwa paundi milioni 150.8 na chama cha soka cha
England FA baada ya kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2016-17.
Msimu wa 2015-16 ulishuhudia
ongezeko kubwa kwa mkataba wa matangazo ya Televisheni ukitoa takriban
Paundi bilioni 2.4 kwa timu 20 zaidi ya msimu uliopita zilipolipwa
Paundi bilioni 1.6.
Timu iliyoshika mkia kabisa Sunderland imepata Paundi milioni 93.471.
Fedha hizo zinatokana na matangazo ya Televisheni, mikataba ya kibiashara sambamba na zawadi.
Post a Comment