WASHIRIKI WA MAFUNZO YA SERA YA GESI NA MAFUTA WAKIWA KWENYE KAZI ZA VIKUNDI
MWAANDISHI WETU
Kukosekana kwa
watendaji wa wizara ya
nishati na madini ngazi
ya chini , Halmashauri na Manispaa ni
miongoni mwa sababu zinazochangia
migogoro katika maeneo yanayochindwa
madini, gesi na Mafuta.
Hayo yamebainishwa kwenye
warsha ya kuwajengea uwezo wadau kuhusu Tasnia ya uziduaji wa gesi
na asili yaliyoendeshwa na Shirika
na Mrengo Correrition kwa ufadhili
wa shirika la hifadhi na
kulinda mazingira (WWF)
yaliyofanyika ukimbi wa chama
cha walimu Lindi.
Akizungumza kwa niaba
ya washiriki hao Mohamedi
Chimbuli alisema kukosekana kwa
wawakilishi wa wizara ya
nishati na madini
ngazi za chini ikiwemo wilaya kunachangia kuweko
kwa migogoro hisiyo isha katika
maeneo ya uchimbaji kwa
kuwa hakuna watendaji wakaribu wanaoweza
kutatua tatizo kwa wakati.
Chimbuli alisema
kama kutakuwa na watendaji
wa wizara hiyo
ngazi ya wilaya
pamoja mchakato wa kuomba leseni ya
uchimbaji pia ianze ngazi
ya vijiji hiyo itasidia
kuondoa migogoro kati
ya wawekezaji na
wananachi.
Saidi Juma alisema elimu
na uzalendo ni unahitaji na
jambo muhimu kwa watanzania ili kuendesha raslimali za nchi
kwa maendeleo endelevu.
Kwa upande wake
makamu mwenyekiti wa Mtandao wa
Mrengo Gottlieb Mpangala alisema
lengo la
mafunzo hayo ni
kuwajengea uwezo wadau
mbalimbali kuhusu masuala ya ushawishi
na utetezi juu
ya ufuatiliaji mapato
na matumizi ya gesi
na mafuta na uchambuzi
wa sera ya gesi
na mafuta Nishati ya
mwaka 2015.
Mpangala alisema mafunzo hayo
yamekutanisha watendaji wa mitaa,maafisa mazingira,mashirika
yasiyokuwa yakiserikali,Madiwani na
viongozi wa dini
WADUA WAKICHANGIA MADA KWENYE MAFUNZO SERA YA GESI NA MAFUTA
MKUU WA MKOA WA LINDI GODFREY ZAMBI AKIWA NA WAFADHILI WA MRADI KAYA MASIKINI TASAF
Post a Comment