0
Rais Rouhani wa Iran ahsinda muhula wac pili wa urais nchini IranHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES/AFP
Image captionRais Rouhani wa Iran ahsinda muhula wa pili wa urais nchini Iran
Kituo cha Televisheni kinachomilikiwa na serikali ya Iran kimempongeza rais anaetetea kiti chake katika uchaguzi wa sasa Hassan Rouhani kwa ushindi katika uchaguzi uliofanyika siku ya Ijumaa.
Huku ikiwa kura zote zimehesabiwa Bwana Rouhani alikuwa amejishindia asilimia 56 hatua iliozuia awamu ya pili ya uchaguzi dhidi ya mpinzani wake mkuu Ebrahim Raisi.
Rais Rouhani aliripotiwa kuongoza kwa kura millioni 14 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ebrahim Raisi mwenye kura millioni 10 kufikia sasa.
Asilimia 70 ya waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura zao.
Awali Ibrahim Raisi alitoa malalamishi akidai kumekuwa na dosari katika uchaguzi huo.
Raisi, ambae anaungwa mkono na kiongozi wa kidini nchini humo , Ayatollah Khamenei, amekuwa akikosea sera za rais Rouhani akisema ameruhusu mwingilio wa nchi za kigeni kuathiri Iran huku kukiwa pia na usimamizi mbaya.
Bw. Rouhani kwa upande wake ametetea sera zake akisema zilimwezesha kuuchipua uchumi kwa kufanikiwa kushawishi kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vilivyokuwa vimewekewa taifa hilo kwa miaka mingi.
Na pia kufanikisha mkataba wa kinuklia jambo ambalo limepunguza uhasama na mataifa ya nje.

Post a Comment

 
Top