Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria.
Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru
kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Ndugu Castory Manase Nkuli
baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000
na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya
Ardhi.
Mhe.
Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi
haukufuatwa na badala yake kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa
ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa
kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa
idhini ya Rais.
Aidha,
Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa
kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na kuisaini kwa niaba
ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa Mipango Miji ili kuimilikisha
kampuni ya Azimio Housing Estate ambalo pia ni kosa kisheria.
Akithibitisha
makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya
Ardhi Bi Immaculate Senje amesema kwamba utaratibu wa umilikishaji wa
ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke
kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wana
kijiji.
“Kama
nyie hamna uwezo wa kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kazi kuanzia
leo hafai kuwa mtumishi wa serkali” alisema Mhe. Lukuvi na kuagiza eneo
hilo lirudi na kuwa mali ya serikali “ Sasa hiyo ardhi lazima irudi
itakua mali ya serikali kuanzia leo” .
katika
ziara hiyo, Mhe. Lukuvi ametembelea ofisi za ardhi Lindi na kufanya
ukaguzi katika Masijala za ardhi na kuangalia mfumo wa ukusanyaji kodi
ya pango la ardhi, kisha kuwaagiza watendaji wa ardhi mkoani hapo
kuhakikisha wanatoa hati kwa wakati na kukusanya kodi ya pango la ardhi
kwa kila mmiliki wa ardhi ili kuongeza pato la serikali.
Pia
alitembelea ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani hapo na
kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa shirika hilo mkoani Lindi Ndugu
Gibson Mwaigomole. Katika taarifa hiyo Mhe. Lukuvi amelishauri Shirika
la Nyumba la Taifa kufanya uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za
kisasa pamoja na Nyumba zenye gharama nafuu.
Aidha,
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akiwa pamoja na waziri Lukuvi
na watendaji wa mkoa ameeleza kuwa sekta ya ardhi mkoani hapo
inachangamoto nyingi lakini ofisi yake inaendelea kufanya jitihada za
makusudi kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa
maslahi ya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto)
wakihakiki nyaraka na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kulia)
katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi,
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi, watendaji na viongozi wa Mkoa
wa Lindi wakiwa katika mkutano wakati wa ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani
Lindi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza
kuhusu utaratibu za upangaji miji na umilikishaji ardhi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi akijieleza
kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.
Godfrey Zambi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akikagua mafaili katika masijala ya ardhi mkoani Lindi ambapo alibaini
mapungufu ya kutokuwa na usahihi wa uwekaji kumbukumbu za ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa
Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi wakikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya
pango la ardhi mkoani Lindi
Ndugu Gibson Mwaigomole Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Lindi.


Post a Comment