Mwenyekiti wa viziwi mkoa wa Lindi, ndugu Jafar
Murtaza.
Mwenyekiti wa viziwi mkoa wa Lindi, ndugu Jafar
Murtaza amewatakia kheri waandishi wa habari katika siku ya
kuadhimisha uhuru wa vyombo vya habari yanayofanyika kimkoa katika kijiji
cha Kiwalala jimbo la mtama mkoani Lindi.
Murtaza ameyasema hayo leo mei 3
alipokuwa akizungumza na Liwale Blogo kupitia mtandao wa kijamii.
“Ndugu zangu waandishi nawaomba katika
siku yenu ya uhuru wa vyombo vya habari tufahamuni sisi ndugu zenu wa
kutosikia (viziwi) hatupati habari kikamilifu na tunakata tamaa kufatilia kazi
zenu kwasababu vyombo vyenu huwa havina wakalimani ambao ndio nguzo yetu
muhimu.,ndugu waandishi ninyi ndio wapashaji habari piganieni haki zenu pia
boresheni huduma zenu za utoaji habari kwa kuibua waandishi ambao ni rafiki wa
wenye ulemavu wa kusikia yaani watafcri moja kwa moja.” alisema Murtaza
Pia aliwataka waandishi wa habari
wasikubali kukandamizwa haki zao na wala kuingiliwa uhuru bila sababu za
kimsingi pia awataka waandishi wa habari kuweka vipaumbele kwa watu wenye
ulemavu ili wafuraie kazi za habari na kuwaunga mkono kutokana na
mchango wao wa kuwapatia habari.

Post a Comment