Baadhi
ya mahabusu wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi jijini Arusha aprili 25 wamegoma
kushuka katika gari la magereza kwa madai kuwa hawatendewi haki kwa kesi
zao kutosikilizwa hali inayowalazimu kukaa mahabusu kwa muda mrefu bila
kujua hatima yao.
Tukio
hilo lilitokea katika viwanja vya mahakama majira ya saa 3:27 asubuhi
ambapo tukio hilo lilisimamisha shughuli za mahakama kwa muda wa zaidi
ya masaa mawili huku baadhi ya watuhumiwa wengine wa ugaidi wakivua nguo
zao kushinikiza kesi zao kusomwa
Mahabusu
32 tu ndio waliokubali kushuka katika gari hilo na kuingia mahakamani
huku 29 wakigoma kushuka na kubakia ndani ya gari hali iliyozua taharuki
kwa baadhi wa watu walikuja kufatilia kesi hiyo na zinginezo.
Hakimu
mkazi wa mahakama hiyo Mhe. Nestory Baro aliwataka watuhumiwa hao kuwa
wavumilivu, kwa kuwa kesi yao ipo katika hatua za mwisho huku akiwasii
kutogomea kuja mahakamini kwa kufanya hivyo wanajinyima haki yao ya
kisheria.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mahakamani hapo baadhi ya watuhumiwa Shabani Idi na
Yusuph Alli waliiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo kwa kuwa familia
zao zinaishi katika wakati mgumu.
“Mtoto
wangu wa darasa la nne amekatisha masomo anaokota makopo kwa ajili ya
kuuza ili familia wapate chakula pamoja na wadogo zake kupata nauli ya
shule”alisema Shabani.
Waliongeza
kuwa familia zao sasa zipo hatarini kuingia katika makundi mabaya ya
tabia kutokana na wazazi wao kuwa mbali nao hivyo wao kuendelea kuwepo
magerezani ni changamoto kubwa sana kwa familia zao
Post a Comment