Jaji wa mahakama
moja katika jimbo la Washington Marekani amekataa kutoa agizo la muda la
kusitisha marufuku mpya ya usafiri iliyotolewa na rais Trump.
Jaji huyo, James Robart, amewataka mawakili wanaowakilisha majimbo yanayopinga marufuku hiyo kutoa ushahidi zaidi.
Wanasema
amri mpya ya Trump dhidi ya raia wa mataifa 6 ya kiislamu si tofauti
sana na marufuku ya awali ambayo jaji huyo alisitisha.
Marufuku
hiyo inafaa kuanza kutekelezwa alhamis ijayo, japo inakabiliwa na
vikwazo chungu nzima vya kisheria kutoka kwa majimbo kadhaa yanayosema
marufuku hiyo inakiuka katiba.
Lakini jaji huyo alisema kuwa ana sababu za kutofanya hivyo.
Amesema kuwa lazima walalamishi wawasilishe ombi kabla ya yeye kutoa uamuzi wake.
Idara
ya haki nchini humo ilikuwa imesema kuwa kwa sababu marufuku ya kwanza
ya uhamiaji ilikuwa imepingwa na mahakama jaji huyo hangeweza kutoa
uamuzi wa moja kwa moja.
Wale wanaopinga maraufuku wanasema kuwa
ina athari sawa na ile ya hapo awali.Wamesemakuwa hatua hiyo ni kinyume
na katiba na inaharibu biashara katika jimbo la Washington.
Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse Sean Spicer amesema kuwa anaamini kuwa agizo hilo jipya litaidhinishwa na mahakama.
Majimbo kadhaa pia yamewasilisha maombi ya kupinga sheria hiyo.
Post a Comment