Dismiss
Bara la Afrika sasa
lina anwani yake ya mtandao .africa sawa na ule wa .com kufuatia
uzinduzi wake rasmi na muungano wa Afrika AU.
Mwenyekiti wa tume
ya umoja huo Nkoszana Dlamini alipongeza uzinduzi wake kama wakati
ambapo Afrika imejipatia utambulisho wake wa kidijitali.
AU inasema kuwa anwani ya .africa utalileta pamoja bara la Afrika kama jamii ya mtandao.
Anwani hiyo sasa itaonyesha maslahi ya makampuni barani Afrika.
- Satelaiti ya kufikisha mtandao kasi Afrika yaharibiwa
- Mtandao wa tume ya uchaguzi Ghana wadukuliwa
- Programu mpya ya Facebook kuzinduliwa Kenya
- Sheria tata za mtindo wa nywele shuleni A.Kusini zasitishwa
- Nana Akufo-Addo ndiye rais mpya Ghana
Kwa mfano kampuni ya simu inaweza kuanzisha anwani yake ya mobile.africa ili kuonyesha uwepo wake barani Afrika.
Icann, kampuni inayotengeza anwani hizo iliiidhinisha hatua hiyo baada ya AU kuwasilisha ombi.
Kampuni hiyo iliongozwa na kampuni ya Afrika Kusini ZA Central Registry ambayo itahusika na usajili wa majina ya .africa.
Post a Comment