Nembo ya mahakama ya kimataifa
Waandishi sita nchini Ivory Coast wameshtakiwa kwa kueneza habari potofu hivyo kuhatarisha usalama wa taifa.
Washtakiwa
hao sita, ni waandishi na wahariri ambao jarida lao limechapisha makala
kuhusu uasi uliofanywa wiki iliyopita na vikosi maalum vya nchi hiyo.
Waandishi hao wameripoti kwamba vikosi maalum viliomba fedha nyingi ili
kusitisha uasi wao.
Lakini serikali imedai wanajeshi hao walirudi
kazini bila kuwepo kwa masharti yoyote, na kuongeza kusema kwamba pia
wanajeshi hao waliomba radhi kwa mgomo wao wa siku mbili uliofanyika
katika kambi ya Adiake karibu na mpaka wa Ghana.
Waandishi hao,
wanaofanya kazi katika gazeti la kujitegemea, wameripoti kwamba wizara
ya ulinzi umewalipa waasi hao kurudi kazini.
Wameachiwa baada ya
kuwepo kizuizini kwa siku mbili. Lakini mashtaka wanayokabiliwa nayo ya
kuhatarisha usalama wa taifa, hukumu yake inaweza kuwa kifungo cha mpaka
miaka mitano. Uasi wa kwanza ulianza mwezi jana katika mji mkuu wa
Bouake na hatimae kuenea nchi nzima.
Post a Comment