Katika
kuangalia tabia za wanawake, kuna hii orodha ya wanawake ambao kama
mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya
mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu
na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii
ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida katika
mahusiano yako nao mbeleni.
1. Mtumiaji
Kuna
aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili
wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume
ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye
unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe
itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata
kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na
kukuacha kwenye giza.
2. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu
ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote
ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba
msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo
alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya
mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu
mzuri wa kuishi naye hata mara moja.
3. Mlalamishi
Huyu
ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na
lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia.
Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku
nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa
kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.
4. Asiyejielewa
Huyu
ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye
atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho
anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia
inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina
hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake
kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina
hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.
5. Anayetawala na kutotosheka
Hii
ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki
kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile
ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni
gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii
ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia
kichwani na wao kujifanya mabosi.
6. Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa
na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika
mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya
wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani
basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya
wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani,
bila hata kufikiria wenzao.
7. Nusa Nusa
Aina
hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila
wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza miondoko yako. Unaweza
kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze
chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda
wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu
nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila
anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona
mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye
ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye
mara moja.
8. Asie na maono
Aina
hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni
kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza
kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo
lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza
kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda
unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake
iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe
ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke
asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.
9. Mcheza ndondi
Hii
ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na
chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya
mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.
10. Mtoto wa mama
Aina
hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi
wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu
mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani
yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza
wazazi wake.
Post a Comment