Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amemteua Rogers Sianga kuwa
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini.
Kamishna Mkuu Sianga
atasaidiwa na Mihayo Msikhela ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Fredrick
Kibuta ambaye anakuwa Kamishna wa Intelijensia.
Wakati huo huo, Mhe. Rais
Magufuli amemteua Dkt. Anna Peter Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Kabla ya uteuzi huo Dkt.
Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Moshi, kilichopo Mkoani Kilimanjaro.
Uteuzi huu unaanza mara
moja na wateule wote wataapishwa siku ya Jumapili Februari 12.
Post a Comment