Siti Aisyah, mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya nduguye kim Jong un
Mwanamke kutoka
Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa
kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90, kushiriki katika
kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.
Wanabalozi wa Indonesia
waliokutana na Siti Aisyah, wanasema aliwaambia kuwa wanaume wawili,
walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa mafuta yaliofanana na yale
ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.
Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati ya sumu kali kabisa.
- Mwili wa Kim Jong-nam walindwa vikali
- Kifo cha Kim: Mwanamke akamatwa Malaysia
- Korea Kaskazini ndiyo ilimuua Kim Jong-nam, yadai Korea Kusini
Maafisa wa polisi wa Malaysia wanasema wataanza kufagia uwanja
huo wa ndege ambapo shambulio hilo lilifanyika siku 12 zilizopita ili
kuchunguza sumu yoyote iliosalia.
Maafisa wa polisi wa Malaysia walivamia nyumba yake huko Kuala Lumpur mapema wiki hii ili kuchunguza mauaji hayo.
- Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong nam akamatwa
- Nduguye Kim Jong-un auawa Malaysia
- Balozi wa Malaysia nchini Korea Kaskazini aitwa nyumbani
Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo ,huku washukiwa
wengine saba waisakwa na polisi ikiwemo raia wanne na Korea Kaskazini
Post a Comment