Na Ibrahim Yassin, Kyela
MKAZI wa Kitongoji cha Njisi, Kijijiji cha Kilwa, wilayani Kyela,
Tummanye Makula (35) , amekaa na ujauzito miezi 13 na kushindwa
kujifungua.
Hata hivyo, baada ya maombezi, alijikuta akijifungua chura na baadaye mdudu wa ajabu akiwa na manyoya meusi.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki baada ya dada huyo kumpigia simu
Mchungaji wa Kanisa la Tample Of Prayer For All Nations Church, Nabii
Charles Mkuvasa wa mjini Kyela akihitaji kuombewa.
Alicuhukua hatua hiyo baada ya kukaa na ujauzito kwa muda wote huo na
kushindwa kujifungua, licha ya kuzunguka kwa waganga wa kienyeji.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Tummanye alisema aliachana na mume wake muda mrefu na kuamua kuishi na mama yake mzazi.
Alisema baada ya miaka miwili, alipata mwanaume mwingine ambaye alimpa
ujauzito huo na siku zote alikuwa akihudhuria kliniki katika Hospitali
ya Wilaya Kyela.
Alisema ilipofika miezi tisa, alipata uchungu siku mbili, lakini
hakujifungua huku madaktari wakimweleza kuwa njia yake ni ndogo, licha
ya kuwahi kuzaa mtoto mmoja.
Baada ya siku mbili uchungu huo ulikata na aliendelea kukaa na
ujauzito wake hadi alipoamua kunywa dawa na kupiga lamri kwa waganga wa
kienyeji, ingawa pia hakufanikiwa lolote, alisema.
Alisema alipokuwa nyumbani aliambiwa na marafiki zake aende kwa Nabii
Charles akaombewe kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutembea na yeye
aliomba namba ya simu na kumpigia.
Alisema Charles alianza kumuombea na baada ya dakika tano, alisikia
uchungu ikabidi aingie ndani…muda mfupi alijifungua chura ambaye
alitoweka katika mazingira ya utata.
“Nilitoka sebuleni na kumweleza mchungaji na mama yaangu nimejifungua
chura ambaye ametoweka katika mazingira ya utatanishi,” alisema.
Alisema baada ya muda mfupi, alijisikia uchungu tena na kwenda chumbani
na kujikuta akijifungua mdudu wa ajabu akiwa na manyoya kama paka na
nywele za rasta, ikabidi amwite mama yake na mchungaji.
Mama mzazi wa Tummanye Makula hakuweza kutaja jina wala kusema
chochote, baada ya gazeti hili kufika nyumbani kwake, isipokuwa alikuwa
akilia tu muda wote.
Mkazi wa Kyela, Bonifas Mwalila, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema tukio hilo ni la kwanza kuliona tangu azaliwe.
Naye Mchungaji Mkuvasa, alisema baada ya kufika kijijini alimkuta mama
huyo akiwa katika hali mbaya, kifo kilikuwa kinamwita lakini kutokana na
maombi alimnusuru.
Diwani wa Kata hiyo, Anna Makula licha ya kukiri kuwapo tukio hilo,
alisema amekuwa akishuhudia matukio mengi ya watu kufika kanisani hapo
wakiwa wamefungwa kamba, lakini baada ya siku tatu alikuwa akishangaa
wakirudi makwao wakiwa wazima.
Chanzo:Mtanzania
Post a Comment