Mahitaji makuu ya mwandamu katika kuishi vyema hapa duniani
anahitaji chakula, mavazi na maradhi, hii ni kwa mujibu ya mwalimu
wangu ambaye aliwahi nifundisha miaka ya nyuma kidogo.
Lakini
tukiachana na mahitaji hayo, hata kwenye mafanikio yapo mahitaji ambayo
ni lazima uwe nayo ili uweze kufanikiwa. Kiuhalisia, itakuwa ni vigumu
sana kama
unataka kufikia ndoto yako kama hautakuwa na vitu vifuatavyo;-
1. Lengo kuu.
Lengo kuu hutokana na malengo mengine madogo madogo. Kama
ilivyo, ili iitwe bahari ni lazima bahari hiyo iweze kupokea maji kutoka vyanzo
vingine vya maji kama vile vijito, mito, mabwawa na mengineyo ndipo itatokea
bahari. Kwa kuona mfano huo tunaweza tuangalie mfano mwingine ambao itatusaidia
kufukia lengo kuu.
Kama unahitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa unahitaji kuwa na
malengo mengine madogo madogo ambayo ndiyo yatakufanya kukamilika kwa lengo
hilo kuu. Hivyo kila wakati ikumbukwe ya kwamba ni lazima uweze
kuyapapalilia vyema malengo yako madogomadogo kwani ndiyo chanzo kikubwa cha
kufikia mafanikio yako.
Hivyo ili uweze kuwa mwenye mafanikio makubwa kwa upande wako
unahitaji kuwa na lengo kuu ambalo litakufanya uwezo kutimiza ndoto yako.
2. Sababu.
Hakuna mafanikio bila ya kuwa na sababu ya kufanya kitu
hicho. Kila kitu unachokiona katika dunia hii kumbuka ya kwamba
mwanzilishi wa kitu au jambo hilo alilianzisha kwa sababu maluumu. Huwezi
kusema unataka kufanya jambo fulani kama huna sababu, kwani mafanikio ya
aina hiyo utawasikia kwa majirani tu.
Hivyo kila wakati kwa kila jambo ambalo unalitaka kulifanya,
kabla ya kufanya jambo hilo kumbuka ya kwamba ni lazima utafute sababu ya
kufanya jambo hilo. Kama hautapata majibu ya kufanya jambo hilo ni vyema
akaliacha kulifanya, kwani kama utaamua kulifanya jambo bila ya kuwa sababu,
jambo hilo litakufa tu baada ya siku chache. Hivyo kumbuka kila kitu
ambacho unakifanya au unataka kukifanya ni lazima kuwe na sababu maalumu.
3. Msukumo wa kiutendaji.
Mafanikio hayajatokea kama ajali kama hakutakuwa na msukumo wa
kiutendaji juu ya jambo hilo. Msukumo humfanya Mtendaji wa jambo hilo
kuweza kutendeka kwa ufasaha kila wakati. Hivyo kila wakati usifanye kitu
kwa sababu mtu fulani amesema ufanye, kwani kama atafanya hivyo
utakosa hamasa ya msukumo juu ya utendaji wa jambo fulani.
Hivyo kuwepo kwa lengo kuu, sababu ya kutenda jambo na
msukumo wa kiutendaji hiyo ndiyo siri kubwa iliyojificha katika kufikia ndoto ambayo
unayo.

Post a Comment