Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imetoa maamuzi
kwa baadhi ya wasanii waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Mahakama hiyo imekubali maombi ya Jamhuri kuhusu tuhuma zinazomkabili
Petitman na wenzake wanne kwamba watakuwa nje kwa dhamana ya shilingi
milioni 20 na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi
kwa muda wa miaka mitatu na kila mmoja anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja
mwaminifu.
Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi
watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni
10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani
Post a Comment