Jaji
mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela
akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini-picha na
Kadama Malunde-Malunde1 blog
Katika kuendana na kasi ya ulimwengu wa sayansi na teknolojia Mahakama
kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga inatarajia kuanzisha mpango wa
kuhakikisha kila hakimu anakuwa na komputa mpakato ili kila hakimu
achape hukumu yake mwenyewe.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Mfawidhi wa Mahakama
kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela wakati wa maadhimisho
ya siku ya sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya mahakama hiyo
mjini Shinyanga.
Jaji Kibela alisema katika kuendana na kasi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) mahakama hiyo inataka kuhakikisha kuwa wananchi
wanapata huduma zinazotolewa na mahakama hiyo kwa wakati ili wapate muda
wa kufanya shughuli zingine za maendeleo ili kukuza uchumi wa nchi.
“Katika matumizi ya TEHAMA mahakama yetu ina mpango wa kila hakimu awe
na kompyuta mpakato ili kila hakimu aweze kuchapa hukumu yake mwenyewe
ili kuongeza kasi ya nakala za hukumu kutolewa ndani ya siku 21.
Katika hatua nyingine Jaji Kibela alisema katika kipindi cha mwaka 2016
mahakama hiyo iliamua jumla ya mashauri 392 yakiwa ni kati ya mashauri
yaliyokuwa yamefunguliwa na yake yaliyobaki mwaka 2015 ambayo kwa ujumla
yalikuwa mashauri 1087.
“Kesi nyingi zimerithiwa kutoka mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora
kabla ya kuanzisha kanda hii mwaka 2015 na pia baadhi ya majaji
wamekuwa na majukumu mengine ya kikazi nje ya kanda.
Naye Kaimu mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea mkoa wa
Shinyanga Paul Kaunda alisema nakala za hukumu hazichapwi kwa wakati n
ahata zikichapwa mahakimu wamekuwa wakitumia muda mrefu kuzifanyia
uhakiki hivyo kuchelewesha azma na haki yam kata rufaa katika mahakama
za juu.
Aidha alisema pia ucheleweshaji wa utoaji haki kwa wakati unasababishwa
na mahakama kuwa na mahakimu wachache kukabiliana na mashuri
yanayofunguliwa kila siku.
Kaunda alilitupia lawama jeshi la polisi kwa kuwashikilia watuhumiwa kituoni kwa zaidi ya saa 24 tangu mtuhumiwa akamatwe.
“Kifungu cha 32 na 33 cha sharia ya mwenendo wa makosa ya jinai
kinawataka polisi wawe wamemfikisha mahakamani mtuhumiwa wa makosa ya
jinai ndani ya masaa 24 lakini cha ajabu mamlaka ya jeshi la polisi
imekuwa ikifanya kinyume na matakwa ya sheeria kwa sababu wanazozijua
wenyewe”,alisema.
Naye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Kahama
Fadhili Nkurlu aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliwataka
baadhi ya watu wanaosema mahakama inaingiliwa na katika majukumu
wapuuzwe.
“Mahakama zetu ziko huru,naombeni muwapuuze watu wanaosema kwamba
mahakama zinaingiliwa,nawaomba pia majaji na mahakimu mtoe haki kwa
wakati kwani tunataka Tanzania mpya yenye haki,sisi tunaposema hapa kazi
tu,basi nyie semeni hapa haki tu”,alisema Nkurlu.
chanzo:Malunde1 blog
Post a Comment