Kila
nchi duniani ina sifa zake kwenye ishu ya hali ya hewa ambapo kwenye
nchi nyingine kuna Joto na kwengine kuna baridi pia wengine wakiwa na
hali ya hewa ya wastani, sasa leo February 7, 2017 nimekukusanyia hizi
sehemu 10 zilizotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha joto duniani.
1.QATAR
Wakati wa
msimu wa joto, nchini Qatar kumeripotiwa kuwa na joto kali na kuna muda
hali ya joto hupanda mpaka kufikia nyuzi joto 50 ambapo pamoja na kuwa
na joto kiasi hicho Qatar imebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini,
mafuta na gesi.
Rasilimali hizi zimeifanya Qatar kuwa nchi ya kwanza duniani kwa utajiri.
2. BOTSWANA
Botswana
inashika nafasi ya pili kwa kuwa nchi yenye joto kali duniani ambalo
linafika nyuzi joto 40 na inaelezwa kuwa 70% ya joto hilo huchangiwa na
jangwa la Kalahari.
3. VIETNAM
Vietnam ni
nchi yenye mfumo wa utawala wa Kisoshalisti kutoka bara la Asia, mji
mkuu wa nchi hiyo ni Hanoi unatajwa katika nafasi ya tatu katika maeneo
yenye joto kali duniani, inaelezwa kuwa kiwango cha chini cha joto ni
nyuzi joto 20 wakati kiwango cha juu kinafikia nyuzi joto 42.
4. UNITED ARAB EMIRATES (UAE)
Umoja wa
Falme za Kiarabu (UAE) unatajwa kuwa kati ya sehemu zenye uchumi unaokua
kwa haraka zaidi duniani, moja ya falme zake (Abu Dhabi) inatajwa kuwa
na joto linalofikia nyuzi joto 45 wakati kiwango cha chini ni nyuzi
joto 25.
5. BAHRAIN
Bahrain ni
moja kati ya nchi ndogo barani Asia, inatajwa kuwa joto lake hufikia
nyuzi joto 40 wakati kiwango cha chini ni nyuzi joto 17.
6. JAMAICA
Jamaica inashika nafasi ya sita katika nchi zenye joto kali ikiwa na kiwango cha chini cha nyuzi joto 27.
7. MALAYSIA
Malaysia
ni moja kati ya nchi za Kiislamu na mji mkuu wake ni Kuala Lumpur wakati
Putrajaya ni jiji kubwa zaidi nchini humo, hali ya hewa ni joto
linaloanzia nyuzi joto 25-35 mpaka kufikia nyuzi joto 40.
8. INDIA
India ni
nchi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu kwenye barala Asia, kiwango
cha juu cha joto kinazidi nyuzi joto 48 wakati kiwango cha chini ni
nyuzi joto 28, ingawa kuna maeneo ya milima hupata baridi mpaka nyuzi 1.
9. INDONESIA
Indonesia
inatajwa kuwa ndio nchi kubwa ya kiislamu duniani na mji wake mkuu ni
Jakarta ukiwa na visiwa vingi huku kukiwa na rekodi ya joto linalofikia
nyuzi 30.
10. ETHIOPIA
Ethiopia
ni nchi ya Kiafrika na mji mkuu wake ni Addis Ababa ambao unatajwa kuwa
na joto linalofikia nyuzijoto 35 wakati kiwango cha chini ni nyuzi joto
25.
Post a Comment