Jitihada za kurejesha miundombinu ya shule ya Msingi
Mlengu kata ya Kigala wilayani Makete iliyoharibiwa na mvua iliyoambatana na
upepo mkali Februari 16 mwaka huu bado zinaendelea
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo Yusto Mwinuka amesema mvua hiyo iliharibu vyumba vitatu vya
madarasa ambavyo ni vya darasa la awali, la pili na la tano, ambapo
wamelazimika kubomoa madarasa yote hayo na kuanza kuyajenga upya
Amesema licha ya changamoto hiyo kuwakumba lakini
wanafunzi wote bado wanasoma baada ya kukarabati chumba kimoja cha darasa
kilichokuwa hakitumiki ambapo sasa kinatumiwa na wanafunzi wa darasa la 5 na
chumba kingine kinatumiwa kwa zamu na darasa la awali na la pili
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kigala Mh Kevin Nguvila
amewaomba wadau wenye moyo kuona namna ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na
wananchi wa kijiji cha Mlengu kuhakikisha madarasa hayo yaliyoezuliwa mapaa
yanajengwa upya ili wanafunzi waendelee na masomo yao kama awali
Amesema kwa hivi sasa tayari ameshakaa na wananchi wake
kuhusu suala la kurekebisha miundombinu hiyo ambao wamekubaliana kuchanga, na
tayari ujenzi wa madarasa hayo upya unaendelea
Sikiliza sauti za viongozi hao(Diwani na Mwalimu Mkuu)
Post a Comment