Ligi daraja na tatu limefungua pazia februari 24 katika
kituo cha Liwale kwa mchezo kati ya timu ya Sido fc dhidi ya Hawili fc mpaka
dakika 90 matokeo yalikuwa sare ya goli 1-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa halmashauri
ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Katika kituo cha Liwale kilikuwa na jumla ya timu mbili zinazoshiriki ambazo zote zilitokea hapa hapa wilayani
ambazo ni Sido fc na Hawili fc hivyo kukosa ushindani mkubwa.
Timu ya Hawili fc ilikuwa ya kwanza kupata goli lililofungwa
na Rehmani Mtipa namo dakika ya 14 goli hilo lilidumu mpaka mapumziko ya dakika
45 kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili Timu ya Sido fc ilibadilisha mchezo
huku ikicheza kutaka kusawazisha goli lakini walizidiwa mbinu za kimchezo
katika dakika ya 75 mchezaji wa Hawili fc,Rashidi Gumbo alijifunga mwenyewe kwa
mpiga kichwa katika harakati ya kutaka kuokoa baada ya kupiga pasi ndefu
Haikosi Mpwate kuelekeza kwenye lango la Hawili fc na kupelekea kupigwa mikwaju
ya penaiti ili kumpata mshindi mmoja.
Hatua ya upigaji wa penaiti ilianza kwa upande timu ya Sido
fc iliweza kupata goli 1 ikikosa penaiti 3 moja akificha mlinzi wa Hawili fc
Masoud huku timu ya Hawili ilipiga mikwaju mitatu na kuweza kutisa nyavu mara
tatu.
Kocha wa timu ya akizungumza na Liwale Blog,Mohamedi Hema
alikili kufungwa katika mchezo huo pia aliweza kuzungumzia juu ya waamuzi wa
mchezo huo alisema waamuzi walichezesha vizuri nae kocha wa Hawili fc,Hasani
Malapo alisema mchezo ulikuwa mzuri kwa pande zote ushindi walioupata ulitokana
na maandalizi mazuri japo ligi haikuwa na changamoto sana kutokana na kituo
kushiriki timu mbili.
Post a Comment