Timu ya Azania
Group, ndiyo itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya
Afrika Mashariki, ya Benki ya "Standard Chartered-Road to Anfield"
yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4.
Azania
walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao
ya 6-5 kwa penati dhidi ya katika mchezo wa kukata na shoka uliofanyika
mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania.Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda.
Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM.
Post a Comment