Wachezaji na viongozi wa Azam Fc
Baada ya Klabu
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kuanza rasmi mazoezi januari 31,2017
jioni kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Ndanda, daktari wa timu hiyo,
Mwanandi Mwankemwa, amezungumzia hali ya kiafya ya baadhi ya wachezaji
waliokuwa majeruhi.
Wengine wanaouguza majeraha, ambao waliukosa mchezo huo ni kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy', kipa Mwadini Ally (nyama za paja) na beki Shomari Kapombe, ambaye ni mgonjwa lakini hivi sasa akiendelea vema.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya jana, Mwankemwa alisema kuwa Bocco na Kingue watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili tokea jana, huku Sure Boy akitarajiwa kuanza rasmi mazoezi leo na Mwadini akipumzishwa kwa siku tatu kuanzia jana.
"Bocco hali yake inaonekana kuimarika vizuri tokea alipopata majeraha hayo ya kuchana msuli wa nyuma ya paja, Stephan (Kingue) kwa upande wake naye amechana msuli wa mbele ya paja, hivyo wote watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili kutoka sasa (jana) na wataanza mazoezi mepesi baada ya wiki moja," alisema.
Daktari huyo bingwa mzoefu, alisema hali za wachezaji wengine ziko vizuri kabisa kuenndelea na mikikimikiki ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za ligi pamoja na michuano mingine.
Post a Comment