0
Ripoti zinasema Bw Kerry Johnson yuko hatarini kutumikia kifungo cha kati ya miaka mitano na 18 gerezani kutokana na mashtaka yanayomkabili.
Ilisemekana alikuwa akicheza Kamari katika kasino ya kifahari ya Mardi Gras lakini akaishiwa na pesa.

Aliondoka na kufululiza hadi katika benki ambapo alimtishia mhudumu kwamba alikuwa na bomu na atalipua benki hiyo kama hatapewa anachotaka.
Kulingana na mashirika ya habari, alifanikiwa kuiba dola 5,000 (Sh515,000) lakini badala ya kutorokea mahali ambapo hangepatikana, alirudi katika kasino kuendelea kucheza Kamari.
Polisi walimkamata siku iliyofuata na upekuzi ulifanywa nyumbani kwake uliwawezesha kupata karatasi iliyofanana na ile aliyoandikia vitisho alivyompa mhudumu wa benki, pamoja na kofia iliyofanana na ile iliyonaswa kwenye video ya CCTV wakati wa wizi.
Inasemekana kulikuwa pia na kitita kikubwa cha pesa zilizofichwa kochini mwake.
Mashirika ya habari yalisema alipofikishwa mahakamani, Bw Johnson alidai alikuwa ametumia dawa siku hiyo na hakuwa anajifahamu, lakini alikiri jamaa aliyeonekana akiiba kwenye video ni yeye.

Post a Comment

 
Top