0
WIZARA ya Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar  imesema, Serikali imeamuwa kuanzisha mfumo mpya wa utowaji wa leseni, pamoja na bodi ya Usimamizi kwa lengo la  kuondowa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.




        Afisa mkuu wizara ya Biashara Zanzibar, Masheko Ali ametoa kauli hiyo alipokuwa akitowa mada ya usimamizi wa mfumo wa utowaji leseni za biashara Zanzibar kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kisiwani  Pemba katika ukumbi wa Makonyo Chake chake, Kusini Zanzibar.
        Masheko Amesema Serikali imeamuwa kuanzisha mfumo huo, kwakua mfumo wa awali unaoongozwa na sheria ya leseni namba 3 ya mwaka 1983 unaonekana sio rafiki, kutokana na kughalimu muda na gharama katika upatikananaji wa baadhi ya leseni.

        Amesema wafanyabiashara wanapaswa kuekewa utaratibu wa aina moja na ulio rahisi wa utowaji wa leseni zao za biashara, ili kuweza kuendesha biashara zao na kuwaletea tija.

        Mapema Afisa uchumi baraza la kusimamia mfumo wa utowaji wa leseni, Hawa Ibrahim Bai amesema kutokana na  Zanzibar kuonekana kuwa na tatizo katika mfumo wa kufanya biashara, Serikali inatilia mkazo kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa lengo la kuleta maendeleo ya kibiashara.

Post a Comment

 
Top