BARAZA la Mji Wete Visiwani Zanzibar limefanikiwa kukusanya, jumla ya shilingi milioni 53, laki 6, 82 elfu, na mia moja sawa na asilimia 64 ya makadirio ya makusanyo shilingi milioni 83,290,000 kwa kipindi cha miezi sita kupitia vianzio vyake vya mapato.
Akizungumza na mwandishi wetu Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Wete Philipo Ntonda amesema kuwa, kati ya fedha hizo
zilizokusanywa, shilingi milioni 36, laki 4, 12 elfu na100 zilitumika kwa kazi za kawaida za kiofisi na shilingi milioni 17, laki 2 na 70 elfu zilitumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumzia mikakati wanayoichukua katika ukusanyaji wa mapato amesema, wanahakikisha wanakuwa na wafanyakazi wenye uwezo, kuwapa hamasa maafisa, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi, wafanyabiashara jinsi ya kulipia ada mbali mbali, leseni usafi na kuwahamasisha kuwa na utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo yao.
Mkurugezi huyo amezitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni, uchache wa wafanyakazi, ambapo hulazimika kuchumoa wafanyakazi wa Idara nyengine kutokana na kustaafu wafanyakazi zaidi ya 21, pamoja na sheria kutoweka adhabu, ingawa tayari wameshapeleka mapendekezo yao kwa Waziri.

Post a Comment