MKUU wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali itahakikisha mikopo inatolewa kwa wanafunzi wanaostahiki na kwa fani zilizopewa kipaumbele huku akiwasisitiza wanafunzi kuepuka udanganyifu na
kuirejesha mikopo hiyo kwa taratibu zilizopo.
Dkt. Shein ameyasema hayo leo huko
katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kilichopo Tunguu
katika Mahafali ya 12 ya Chuo hicho.
Amewataka wanafunzi kuendelea kuitumia vizuri mikopo inayotolewa na kuwa
waadilifu, ili huduma hizo muhimu zinazotolewa ziwe endelevu na ziwe na manufaa
zaidi kwa maendeleo.
Amesema, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa wanaopewa mikopo hiyo
wanakidhi viwango vilivyowekwa na kutumia
fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wa sekta ya umma wanaotaka kusoma kuziomba
taasisi zao kuwasomesha na si Bodi ya Mikopo ya Zanzibar kwani huo ndio uamuzi wa Serikali.
Nae Makamu Mkuu wa SUZA, Profesa Idrisa Rai, amesema wahitimu wa mwaka wa
masomo 2015/2016 katika ngazi mbali mbali za masomo ambapo wanafunzi 861
wamehitimu mwaka huu kwenye masomo 23 ikiwa ni ongezeko la wahitimu 170 na
ongezeko la masomo 8.
Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma ameeleza
mashirikiano yaliopo kati ya Wizara yake na Chuo hicho na kupongeza mafanikio
yaliopatikana.
Post a Comment