SERIKALI ya mapinduzi
Zanzibar imewataka vijana wanaopata fursa ya kufanya kazi nje ya nchi kuhakikisha
taarifa zao zinaifikia Serikali kabla ya kuanza kutumikia majukumu yao.
Waziri wa kazi,
uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto
Moudlin Castiko ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Mwanakwerekwe, Zanzibar kuhusu ziara yake ya siku tano
nchini Quatar, na kukutana na maafisa mbalimbali wenye dhamana ya masuala ya
kazi, mawasiliano na uchukuzi.
Amesema wamekubaliana
kuongeza fursa nyingi
za kazi katika sekta ya
ufundi, madawa, kazi za hudma , ulinzi na ujenzi
pamoja na masuala ya anga
kutokana na taifa hilo kuwa na fursa nying
za ajira.
Amefafanua kuwa
kwa mujibu wa
mkataba na taratibu zilizokubaliwa, vijana watakaopata fursa za
ajira malipo ya
usafiri, viza na mambo mengineyo yatalipwa
na waajiri au
serikali ya Qatar.
Mhe. Castiko ameongeza
kuwa tayari viza za madereva
100 zimeidhinishwa na baaada muda
mchache zitakamilika na
kuwapeleka vijana hao
nchini humo.
KUNA vijana wa
kitanzania wasiopungua elfu moja wanafanya kazi nchini Quatar.
Post a Comment