Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la
Mapinduzi Dr Ally Mohamed Shein amesema njia pekee ya kutoa nchi ni kushiriki uchaguzi
wa huru na wahaki na si kwanamna nyengine yeyote kama baadhi ya watu
wanavyodhania
Dr Shein ameyasema hayo jana wakati akifunga kampeni
wa uchaguzi mdogo wa jimbo la dimani kwa mgombea wa chama cha Ccm ambapo amesema
Nchi na watu wake wataendelea kuishi kwa Amani kwakua hakuna mtu yeyote atakaeweza kuitoa serikali
yake madarakani kwakua ipo kwa mujibu wa sheria za Nchi
Hata hivyo Dr
Shein amewataka wananchi Kuiunga mkono
Serikali na kuacha kusikiliza viongozi wenye lengo la kuwagombanisha na
serikali yao kwakua uchaguzi huru na haki uliopelekea yeye kuwa mshindi wa kiti
cha urais umekwishamalizika na
hakutokuwa na uchaguzi mwengine mkubwa hadi mwaka 2020.
Katika hatua nyengine Dr Shein Amesema tatizo la
ajira ni tatizo la Dunia nzima hivyo Serikali yake imejipanga kulitatua tatizo hilo
kwa kutafuta wawekezaji kutoka nje na ndani ya nchi kwa lengo la kutengeneza
Viwanda vitakavyozalisha ajira kwa wingi hapa nchini
Post a Comment