Rais wa Marekani
Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais, baadhi yake yakiwa ni
ya kubadili yale yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama.
Muda
mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bw Trump, alitia
amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na
gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama
Obamacare, ambayo Trump aliahidi kufanyia marekebisho.
Trump
pia ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri wake wapya wa Ulinzi na
usalama wa kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la seneti.
Utawala
wa Trump pia umeaanza kufanyia marekebisho mtandao wa kijamii wa Ikulu
ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa kipaumbele na uongozi
huo mpya.
Watakoma Hao ahaha
ReplyDelete