Waziri wa Kilimo
Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rashid ametoa rai kwa taasisi husika
kuwaelimisha wananchi kuhusiana na ufugaji wa viumbe vya baharini pamoja kilimo
cha mazao ya baharini kama vile mwani.
Akizungumza
na wanachama wa kikundi cha ushirika wakulima hai kinachojihusisha na ufugaji
wa majongoo ya baharini huko Kilimani mjini Unguja, amesema hatua iliyofikiwa
na kikundi hicho chenye mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ni ya kupigiwa mfano
kutokana kutekeleza adhma ya Serikali kwa wananchi kutumia rasilimali za
Baharini kujikwamua kiuchumi.
Aidha
ameahidi kushirikiana na viongozi wa kikundi hicho kuhakikisha wanapata usajili
wa kikundi chao, kuwatafutia masoko ya kuuza bidhaa zao pamoja na kuwasaidia
kupata mikopo katika taasisi za kifedha ikiwemo mabenki.
Post a Comment