0
Mkuu wa vipindi Bahari fm visiwani Zanzibar, Raya Charles Bonifas(Madam Raya) ameupokea kwa masikitiko makubwa  msiba wa Mwandishi wa Habari wa kampuni ya Uhuru Pablication, Amina Athumani.

                                    Meneja wa vipindi bahari fm Visiwani Zanzibar   
 

Amina, mwandishi wa magazeti ya Uhuru, na Burudani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akizungumza na Liwale Blog ofisini kwake Migombani visiwani hapa Madam Raya amesema kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Bahari Fm radio,Uhuru fm na  kampuni ya Uhuru Pablication msiba huo umewagusa  kwakiasi kikubwa na pia ametumia nafasi hii kutoa salaam za pole kwa mkuu wa Vipindi Uhuru fm na Uongozi mzima wa Uhuru Pablication

 "kiukweli msiba huu ni wakwetu wote maana sisi(Bahari fm, Uhuru fm na  kampuni ya Uhuru Pablication sote tupo chini ya chama cha mapinduzi CCM, hivyo ni kitu kimoja na hata utendaji kazi wetu tunategemeana kwa kiasi kikubwa hivyo wafanya kazi wa bahari fm sote tunaungana na familia ya marehemu, ndugu jamaa pamoja na tasnia nzima ya waandishi wa habari nchini katika kuomboleza kifo chake,"amesema Madam Raya.


mwandishi wa magazeti ya uhuru, na burudani amina athumani enzi za uhai wake


Katika hatua nyengine Raya, umesema kwamba Amina alilazwa kwenye hospitali hiyo baada ya kuzidiwa kutokana na kushikwa uchungu, ambapo alijifungua mtoto wa kiume, lakini kwa bahati  mbaya alifariki.

Baada ya mtoto kufariki, Amina aliendelea kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkumba leo asubuhi katika Hospital ya Mnazi mmoja Visiwani Zanzibar.

Marehemu Amina alikwenda Zanzibar kikazi kwa ajili ya kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, yaliyomalizika Ijumaa iliyopita.
mwili wa marehemu Amina unatarajiwa kusafirishwa kesho kutoka visiwani Zanzibar kuelekea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli za kuaga,  kabla ya kuusafirisha mwili kuelekea nyumbani kwao Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwaajili ya mazishi


Post a Comment

 
Top